Waziri wa Afya nchini Congo, Jean Jacques Mbungani amethibitisha kisa kimoja cha Ebola Mashariki mwa Taifa hilo, ikiwa ni miezi 5 baada ya mlipuko wa hivi karibuni kuisha.
Bado haijafahamika ikiwa kisa hicho kinahusiana na mlipuko wa 2018 – 2020 ambao ulipelekea vifo vya watu zaidi ya 2,200.
Aidha, Mtoto wa miaka 3 ambaye amefariki dunia alibainika kuwa na Ugonjwa huo huku watu wapatao 100 wamewekwa katika uangalizi kuona kama wataonesha dalili zozote.