Serikali ya Jimbo la California nchini Marekani imetia saini mswada unaopiga marufuku kuvua kondomu wakati wa tendo la ngono bila makubaliano kuwa sheria.
Hali ya kutoa kondomu bila idhini husababisha madhara ya muda mrefu ya kimwili na kihisia kwa waathiriwa.
Mswada huo uliowasilishwa kwa jina “stealthing”, ulitiwa saini na Gavana wa jimbo la California Gavin Newsom.
Sheria hiyo mpya inaelezea utoaji wa kondomu bila makubaliano ya wanaojamiana kama unyanyasaji wa kingono.
Sheria hiyo mpya imeongezwa katika kipengele cha sheria ya jimbo hilo kuhusu ngono ikielezea utoaji wa kondomu bila makubaliano ya wanaojamiana kama unyanyasaji wa kingono.
California sasa ni jimbo la kwanza la Marekani kuidhinisha utoaji wa mpira wa kondomu bila ruhusa kuwa kosa linaloadhibiwa kisheria.
Kulingana na Cristina Garcia aliyewasilisha mswada huo bungeni, hali ya kutoa kondomu bila idhini husababisha madhara ya muda mrefu ya kimwili na kihisia kwa waathiriwa.
Sheria hiyo inawapatia walalamisi nafasi ya kuwasilisha mashtaka yao iwapo wananyanyaswa kingono.