Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wapatao 16 ambao ni Raia wa Ethiopia wameshikiliwa katika Mji Mkuu wa Addis Ababa, Msemaji wa Serikali amesema wamekamatwa kwa kushiriki kwao katika vitendo vya kigaidi.
Hivi karibuni Ethiopia imetangaza hali ya hatari, baada ya mapigano ya mwaka mzima kuzidi kupamba moto na watu wa kabila la Tigray wakizidi kukamatwa kiholela, Watu wote 16 waliokamatwa wana asili ya Tigray.
Kwa upande wake Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema Umoja wa Mataifa haukupewa sababu za kukamatwa kwa Wafanyakazi hao lakini Watigray ikiwa ni pamoja na Wanasheria, wanasema kumekuwa na matukio ya ukamataji wa kikabila.