Waziri wa Nishati, January Makamba asema Mkurugenzi wa TPDC, Dkt. James Mataragio atatakiwa kutoa maelezo baada ya kusema mafuta yaliyopo yanatosha kwa siku 15 tu
“Hakuna uhaba wa mafuta nchini. Hakuna sababu ya kuwa na taharuki. Utaratibu wa kuingiza mafuta unahakikisha kwamba mahitaji yapo wakati wote. Serikali inaendelea kuchukua hatua kuongeza uhakika wa upatikanaji na unafuu wa bei” Makamba
Akijibu swali la mdau alieuliza mkanganyiko kati ya mkurugenzi wa TPDC na kauli yake kujichanganya, Makamba amesema yake ni Kauli ya uhakika ya Serikali.
Mkurugenzi wa TPDC atatoa taarifa kuhusu taarifa yake kwasababu aliitoa kwenye semina ya wanahabari lakini ni gazeti moja tu ndio limeandika. Pia amemtaka mkurugenzi wa TPDC aende ofisini kutoa maelezo kabla hajachukuliwa hatua za ziada.