Ni Healdines za Platform ya ku stream muziki yaani Apple leo Novemba 30, 2021 wametangaza majina ya wasanii walioshindi tuzo mwaka 2021.
Sasa hivi wameongeza vipengele vitano ambavyo wamevipa jina la New Regional Artist of the Year awards na katika vipengele hivyo vipya washindi waliotajwa ni Aya Nakamura (France), OFFICIAL HIGE DANDISM (Japan), RIN (Germany), Scriptonite (Russia), and Wizkid (Africa).
Hapa nimekusogezea orodhaa kamili ya washindi waliotajwa.
1.Global Artist of the Year
The Weeknd ametajwa kushinda kipengele cha Global Artist of the Year yaani ni ndio msanii pekee alieongoza kusikilizwa mwaka huu kupitia platform yao ya Apple.
Kwa mujibu wa Apple wanasema The Weeknd amekuwa ni msanii ambae tangu alipoachia ‘Blinding Lights’ imekuwa ikishika namba 1 kupitia Top 100 ya Global Chart.
2.Breakthrough Artist of the Year, Album of the Year, and Song of the Year:
Olivia Rodrigo ni binti mwenye Umri wa miaka 18 ambae ameshinda tuzo tatu katika vipengele tofauti ikiwemo Breakthrough Artist of the Year, Album of the Year, and Song of the Year na unaona hapo juu pichani akiwa amezshikilia tuzo zake tatu ni Mmarekani huyo.
3.Songwriter of the Year: H.E.R.
H.E.R ni msanii kutokea Marekani ambae ametajwa kushinda tuzo ya Songwriter of the Year yaani mwandishi bora wa mwaka kupitia platform ya Apple mwaka huu 2021.
H.E.R ni miongoni mwa wasanii wadogo wanaoangalia kwasasa nchini Marekani kutokana na uimbaji wake pia namna nyimbo zake zina jumbe tofauti.
Kwasasa ameachia album yake mpya iitwayo Back of my Mind na miongoni mwa nyimbo zilizopata stream sana kupitia Apple ni Damage pamoja na ile aliyomshirikisha Chris Brown iitwayo Come through.
4.Artist of the Year (Africa): Wizkid
Wizkid ametajwa kushinda tuzo ya Msanii bora kutokea Afrika alieongoza kusikilizwa zaidi kupitia platform ya Apple mwaka huu.
Na kwa mujibu wa Apple wameitaja ngoma yake Essence aliyomshirikisha Tems ambayo imesikilizwa na watu Milioni 125 kupitia Platform yao pamoja na kuuliziwa kupitia mtandao wa Shazam watu Milioni 2.8 na mengineyo zikiwemo shows zake
5.Artist of the Year (France): Aya Nakamura
Aya Nakamura mara kadhaa uingia katika vipengele vya tuzo katika nchi mbalimbali Afrika na time hii ametajwa kushinda tuzo ya Artist of the Year (France) ni mzawa wa Ufaransa na kama unavyoona picha akiwa ameshikilia tuzo yake.
6.Artist of the Year (Germany): RIN
NI Rapper kutokea nchini Ujerumani ambae ametajwa kuwa msanii bora wa mwaka alieongoza kwa mwaka kwa kusikilizwa kwa mwaka kupitia platform ya Apple.
7.Artist of the Year (Japan): OFFICIAL HIGE DANDISM
Ni kundi kutokea Japan linaitwa Official Hige Dandism ambao wao wametajwa kushinda tuzo ya msanii bora wa mwaka na kama unavyowaona katika picha yao ya pamoja wakiwa wameishika tuzo yao.
Artist of the Year (Russia): Scriptonite
Ni Scriptonite ambae ametajwa kushinda tuzo ya msanii bora wa mwaka kutokea nchini Russia aliesikilizwa zaidi nyimbo zake kupitia platform ya Apple.