Mwimbaji Staa wa Bongofleva Juma Jux ambaye pia ni Mfanyabiashara, usiku wa kuamkia leo amezindua duka ambalo litakua likiuza mavazi ya brand ya African Boy ‘African Boy Store’ Sinza Afrikasana Dar es salaam, hii ni dalili nzuri ya ukuaji wa biashara na brand yake ambayo kwa miaka yote hiyo zaidi ya 6 hakuwahi kuwa na duka bali alikua akiuza mavazi yake kwenye maduka ya Watu wengine.
Kwenye siku hii kubwa Mastaa mbalimbali walikuwepo akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Nickson Simon ‘Nikk wa II, Joh Makini, Ommy Dimpoz, Marioo, Ben Pol, Shilole na wageni waalikwa wengine na @AyoTV_ pia imenasa kila kitu kuanzia nje ya duka mpaka ndani ya duka.