Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issa, amesema Mtoto anayefahamika kwa jina la Evancy Underson mwenye umri wa miaka 13 aliemaliza Shule moja ya Msingi, Makambako amejinyonga kwa kamba ya katika eneo la jikoni baada ya kukasilishwa na kitendo cha Baba yake kumuonya juu ya upotevu wa fedha.
“Mtoto alipomaliza Shule akawa anamsaidia Baba yake kuuza Duka Makambako, Baba yake akaona hesabu kama haziko sawa akamwambia Mtoto kama unaiba hela uache, Mtoto akapata hasira na kujinyonga, Dada yake alikuja akakata kamba na Mtoto akakimbizwa Hospitali lakini alifia njiani”
“Inasikitisha sana, Wazazi nendeni taratibu na hawa Watoto wenu na Watoto pia mmomonyoko wa maadili umekuwa mkubwa maaana Mtoto kama huyu kujinyonga inashangaza, alikuwa anajiandaa kwenda Form One mwakani ndoto zake zimekatika”