Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema vikwazo katika Huduma ya Afya vilivyotokana na janga la COVID-19 vimepelekea vifo 69,000 zaidi vya Malaria mwaka 2020, ikilinganishwa na mwaka uliopita
Takriban watu 627,000 ulimwenguni, wengi wao watoto wadogo kutoka Mataifa masikini ya Afrika walifariki dunia kutokana na Malaria mwaka 2020 wakati idadi ya mwaka 2019 ilikuwa 558,000
Wataalamu wanatarajia mapambano dhidi ya Malaria yanaweza kuimarika baada ya WHO kuidhinisha Chanjo ya RTS, S (Mosquirix) na kupendekeza itolewe kwa Watoto Barani Afrika.