Watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazopatikana kwa njia za kidigitali hususani kupitia mfumo mpya uliozinduliwa wa ACEX ukifanya kazi kama gulio la kidigitali hivyo kufanikisha biashara ya ununuzi na uuzaji wa fedha za kigeni, sarafu za mtandaoni, hatifungani na bidhaa mbalimbali za kifedha kwenye soko la kifedha barani Afrika na kwingineko duniani.
Mfumo huu wa kidigitali utawawezesha wawekezaji katika soko la ardhi na makazi, utafiti na uchimbaji wa madini, masuala ya mitaji, mikopo midogo midogo, mifumo ya malipo huku wawekezaji wakipata magawio kupitia biasha hizo.
Kulingana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa ACEX, Bwana. Peter Mucheru jukwaa hili la aina yake linaandikwa upya historia ya Afrika kwa kufanya mapinduzi ya aina yake katika uchumi wa kifedha uanotumia njia za kidigitali.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hii wakati wa uzinduzi wa jukwaa hili mjini Nairobi hivi karibuni, ofisa mtendaji huyo alisema ACEX litakuwa jukwaa la kwanza ambapo wawalishaji wazawa wataweza kusajili bidhaa za kupanga bei za ushindani na kupata faida moja kwa moja kupitia juhudi zao.
“Tunao pia mfumo wa huduma ndogo za kifedha ambao tunaweza kushirikiana na taasisi ndogo ndogo za kifedha za nchi husika na kuziwesesha kifedha ili ziweze kutoa mikopo kwa wenye biashara ndogondogo na za kati”, alisema.
Bwana Muchechu alisema kwa sasa wanaendelea kufanya majadiliano na taasisi ndogondogo za kifedha nchini Tanzania na maafikiano yakipatikana kulingana na taratibu, sheria za kifedha nchini humo wataweza kuziwezesha taasisi hizo kimitaji.
“Tunafahamu kuwa kuna tatizo kubwa la uelewa miongoni mwa watu linapokuja suala la uchumi wa kidigitali, hasa katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki, wengi wakiogopa kutapeliwa na wezi wa mitandaoni, jukwaa letu litatoa elimu na kwa kupitia wawakilishi wetu wakazi tutahakikisha kila mmoja anapata ufahamu wa kutosha kabla ya kuanza biashara”, aliongeza.
Ofisa huyo aliongeza kuwa kwa sasa Temcoin ($XTEM), ndiyo sarafu mama ya kidigitali kwenye soko la ACEX ikitumika katika shughuli mbalimbali za kifedha ikiwa na mfumo wa kasi na wenye ufanisi na ni sarafu yenye sifa ya kupunguza gharama za biashara.
Naye mmoja wa wafanyabiashara kwa kutumia mtandao wa jijini Dar esSalaam, Bwana Elibariki Shilla ambaye ana uzoefu mkubwa wa kupitia mahusiano yake na Kampuni ya TE Markets inayoratibu jukwaa la ACEX aliwataka wadau na wawekezaji nchini kutumia fursa zinazopatikana katika jukwaa hilo kwani linatoa chaguzi tofauti za kufanya biashara kuliko majukwaa mengine duaniani.
“Kwa wale wenye hofu ya kufanya biashara mtandaoni kuna wataalamu wanaotoa elimu ya jinsi gani ya kufanya biashara hizo hivyo na pia kwa kufuata hatua kwa hatua kama wafanyavya wafanyabiashara waliothibitishwa”, alisema.
Naye mjasiriamali mwingine wa mtandaoni wa jijini Dar es Salaam alitoa changamoto hasa kwa vijana kutumia mitandao vizuri ili kujipatia kipato na kuondokana tatizo la kukimbilia ajira mara baada ya kumaliza masomo.
“Kikubwa tu nasisitiza watu wapate elimu, baada ya kupata elimu hapo ndipo mtu anaweza kutengeneza pesa kupitia majukwaa ya mitandao mbalimbali. Hata serikali yetu ilituasa vijana kutumia TEHAMA vizuri ili tuweze kujikomboa kiuchumi”, alisema.
Katika jukwaa la ACEX kutakuwa na watu waliothibitishwawatakaojulikana kama Wakala atakayeruhusiwa katika biashara ya
kubadilisha sarafu ya kidigitali ya $EXTEM kuwa pesa halisi ya nchi husika au kinyume chake.
Kulingana na ACEX, wakala hawa watapatikana Afrika nzima ili kuwezesha utekelezaji bora, salama na sahihi wa miamala ya kifedha kwa ada nafuu. Mawakala hawa watahusika pia na utatuzi wa masuala yanayohusiana na uhamishaji wa fedha Barani Afrika.