Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) ambaye amehitimu hivi karibuni aliyefahamika kwa jina la Magreth Mashue ameuwawa na watu wasiojulikana huku chanzo kikikwa bado hakifahamiki.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) mkoa wa Morogoro, Ralph Meela amesema kuwa Msichana huyo alikua anasona Chuo kikuu Cha SUA Kozi ya Sayansi ya Mazingira na kufanikiwa kufanya mahafali Novemba 26, 2021 na Disemba 14 alipotea hadi Disemba 18 mwili wake ulipopatikana katika mashamba ya Chuo hicho.
Meela anasema uchunguzi wa awali unaonesha shingo ya marehemu imelegea huenda ikiwa ndo chanzo cha kifo chake huku upelelezi ukiendelea kuwabaini waliohusika na kifo chake.
Amesema hadi sasa wanamshikilia mtu mmoja katika tukio hilo ambaye alikua rafiki yake wa kiume.
Kaimu Afisa Mawasiliano Hospitali ya Rufaa mkoa Morogoro, Scolastika Nduga amekiri kupokea mwili wa marehemu, huku Kaka wa marehemu Denis Mashue akiliomba Jeshi la Polisi kuwatafuta waliofanya tukio hilo ili wachukuliwe hatua za kisheria.