Japan imewanyonga Wafungwa watatu leo hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa hukumu ya aina hiyo kutekelezwa ndani ya miaka miwili, huku Serikali ikisema ni muhimu kuendelea na adhabu ya kifo angali bado uhalifu wa kikatili unaendelea.
Msemaji wa Wizara ya sheria ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mmoja kati ya walionyongwa ni Yasutaka Fujishiro mwenye umri wa miaka 65 ambaye alitumia nyundo na kisu kumuua Shangazi yake wa umri wa miaka 80, Binamu zake wawili na Watu wengine wanne mwaka 2004.
Wafungwa wengine wawili ni Tomoaki Takanezawa (54) na Mshirika wake Mitsunori Onogawa (44) waliowaua Makarani wawili katika jumba la michezo mwaka 2003.
Japan ni moja ya Nchi chache zilizoendelea ambazo bado zinatoa hukumu ya kifo ambapo adhabu hiyo inaungwa mkono kwa kiasi kikubwa na Wananchi licha ya ukosoaji wa kimataifa kuwepo.