Mwanamuziki nyota wa kundi la Sauti Sol la nchini Kenya Bien Aime anadai ameiibiwa kwenye tamasha la ‘NRG Wave’ lililofanyika usiku wa mkesha wa Mwaka Mpya katika viwanja vya Carnivore mapema Jumamosi ya Januari mosi 2022,
Bien ameutumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuweka bayana namna tukio hilo la kuibiwa lilivyotokea kwa kusema kwamba alinyakuliwa na kupoteza simu pamoja na funguo za gari yake na vitu vingine vya thamani alivyopteza.
“Simu hiyo ilikuwa na sauti zangu zote za albamu inayofuata ya Sauti Sol,” aliandika.
Na kupitia ujumbe wake aliouweka kwenye mtandao wa Twitter. Bien ametangaza zawadi ya Ksh.50,000 ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 1 za Kitazania, kwa yeyote atakayefanikiwa kurejesha bidhaa zote alizopoteza.