Watoto wawili wa Donald Trump wamekataa kutoa ushahidi wa uchunguzi wa ulaghai katika biashara ya familia hiyo.
Donald Jr, 44, na Ivanka, 40, waliamriwa kutoa ushahidi na Mwanasheria Mkuu wa New York Letitia James.Alifungua uchunguzi wa kiraia mnamo 2019 kwa madai kwamba – kabla ya kuchukua ofisi – Bw Trump alikuwa ameongeza thamani ya mali yake kwa benki wakati akitafuta mikopo.
Mawakili wa Bw Trump wanajaribu kumzuia Bi James kumhoji rais huyo wa zamani wa Marekani na watoto wake.Wamemwomba jaji kufuta ombi “isiyokuwa ya kawaida na isiyo ya kikatiba” ya kutoa ushahidi wao.
Kwa habari kamili na nyingine nyingi fuatilia taarifa yetu ya habari ya Channel Ten Saa 12:00 Asubuhi, saa 7:00 Mchana na Saa 1:00 usiku.