Jeshi la Pakistan limethibitisha kununua ndege za kivita za J-10 kutoka China ikiwa ni mwitikio wa kuimarisha jeshi lake katika upinzani na jeshi la anga la India.
Msemaji wa Jeshi Meja Jeneralk Babar Iftikhar ameuambia mkutano na wanahabari kwamba hatua hiyo ni kuboresha jeshi la anga, na kupata vifaa vya teknolojia nzuri kwa sababu wanafahamu ni teknolojia ya namna gani inatumika na upande mwingine akimaanisha India.
J-10 ni ndege yenye injini moja ambayo inaripotiwa kutumiwa na jeshi la ukombozi la watu wa China toka mwaka 2005. Meja Jenerali Iftkhar amezungumza zikiwa zimepita siku kadhaa baada ya waziri wa mambo ya ndani wa Pakistan Sheikh Rasheed Ahmad kuweka hadharani ununuzi wa ndege za China katika hafla ya umma, akisema ni kukabiliana na hatua ya China kununua ndege za Kifaransa.
Mkataba wa ununuzi wa ndege za kivita 36 ulitangazwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015.