Waziri wa Utamaduni wa Uingereza Nadine Dorries amesema serikali itasimamisha kwa kipindi cha miaka miwili ada ya leseni ya Sh 498,780 au £159 ambayo kila kaya hulipa kwa Shirika la Utangazaji la BBC kila mwaka .
Akizungumza katika Baraza la Commons Jumatatu, Bi Dorries alisema serikali haiwezi “kuhalalisha shinikizo la ziada kutoka katika familia zinazofanya kazi kwa bidii.”
Ada ya leseni hulipwa na kila kaya kupata huduma za BBC ikiwa ni pamoja na TV, redio, tovuti ya BBC, podikasti, iPlayer na programu zingine.
Mpango wa ada umeweka na Katiba ya Kifalme na unatarajiwa kuendelea hadi angalau Desemba 30, 2027, lengo ikiwa ni kufadhili shughuli za BBC.