Mwanamume mmoja ameuawa kwa kupigwa mawe na umati wa Watu, kwa tuhuma za kuchoma kurasa za Quran nchini Pakistan, tukio ambalo limetafsriwa kuwa ni kufuru.
Polisi wanasema zaidi ya Watu 80 wamekamatwa wakihusishwa na mauaji hayo ya Jumamosi katika Wilaa ya Khanewal Mkoani Punjab.
Mwanaume huyo alikuwa chini ya ulinzi wa Polisi kabla ya Umati wa Watu kumteka nyara na kumpiga hadi kufa na kisha mwili wake ulikabidhiwa kwa Familia yake na akazikwa jana Jumapili, february 13,2022.
Munawar Gujjar, Mku wa Kituo cha Polisi cha Tulamba, ambapo kisa hicho kilitokea, amesema Mwanaume huyo aliyechana Quran alikuwa na matatizo ya akili, kwa zaidi ya miaka 15.