Mshtakiwa namba tatu aitwae Waziri Selemani ambae yupo kwenye kesi inayomkabili Mwanamke Wendi Mrema anayetuhumiwa kumuua Mama yake akishirikiana na Waganga wawili na kisha kuuzika mwili nyuma ya nyumba Rau, Moshi, Kilimanjaro amesema alikamatwa bila kujua kosa lake hivyo anaomba Mahakama imuachie.
Wendi Mrema pamoja na wenzake wawili walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza january 26,2022 kwa tuhuma za kumuua Mama aitwae Patrician Ibreck baada ya kuchukua pesa zake za mafao wakidai watamtibu kutokana na kuugua kwake kwa muda mrefu.