Mbunge wa Tanga na Waziri wa Afya Ummy mwalimu amesema Tamasha la Tanga Utalii Festival karibu Mahabani litakuwa linafanyika kila mwaka kwa lengo la kutangaza fursa mbalimbali za utalii na utamaduni wa watu wa Tanga.
Waziri Ummy amesema hayo alipotembelea viwanja vya urthi ambapo tamasha hilo limefanyika leo mwaka huu.
Amesema Tamasha hilo litaboreshwa zaidi na kuongeza siku ili watu wengi kutoka maeneo ya nje ya Tanga waweze kushiriki na kujionea fursa mbalimbali Italii na uwekezaji
” Mbali na kuwa Tanga mji wa mahaba lakini pia tuna mambo mengi ya kuyatangaza kama vile utamaduni wetu, fursa za utalii tuna magoroto ni sehemu nzuri, mapango ya amboni chemichemi za majito hivi vyote vinatakiwa kutangazwa.” Amesema Waziri Ummy.
Aidha amewataka wajasiliamali wa Tanga kulitumia tamasha hilo vizuri kutangaza Bidhaa zao na kupanua masoko.
Kwa upande wa meneja wa tasisi ya Utalii magoroto Jerry Mchechu iliyopo wilayani Muheza Mkoani hapa ameipongeza Serikali kwa kuona umuhimu wa kutangaza fursa za utalii kupitia tamasha hilo.
” Kwakutumia tamasha hili naamini mambo mengi yatafunguka tanga tuna vivutio vingi tuna fukwe za Bahari mapango ya amboni lakini pia utamaduni wa watu wa Tanga utatangazwa ” amebainisha Jerry.
Aidha Jerry amezunguzia utalii wa kilimo cha viungo ambao unapatikana Magoroto Muheza ni fursa nzuri ambayo pia inawainua kiuchumi wananchi wa eneo hilo.
” Katika kuboresha utalii wa kilimo cha viungo tunawawezesha mbegu bora wakulima wadogo wanaoishi kuzunguka eneo la utalii la magoroto ili waweze kujikwamua kiuchumi ” amesema Jerry.
Mwisho