Wiki kadhaa baada ya kuondokewa na wachezaji wake wawili Frank Domayo na Didier Kavumbagu, klabu ya Yanga imeamua rasmi kujidhatiti kwa ajili ya msimu ujao.
Taarifa kutoka Yanga zilizothibitishwa na mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye aligoma jina lake kutajwa zinasema kwamba, beki wa kimataifa wa Rwanda Mbuyu Twite ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia klabu hiyo aliyojiunga nayo misimu miwili iliyopita.
Twitte alikuwa akiwania na vilabu kadhaa vya ligi kuu vikiwemo Azam FC na Simba SC.