Msanii mkongwe kutoka nchini Benin Angelique Kidjo mwenye umri wa miaka 60 ameibuka mshindi wa tuzo ya #Grammys kwenye kipengele cha “Best Global Music Album” kupitia album yake iitwayo Mother Nature na kumpiga chini Wizkid ambaye pia alikuwa anawania naye kipengele hicho na wengineo.
Hii inakuwa ni tuzo yake ya tano ya Grammy katika maisha yake na katika mahojiano baada ya kushinda tuzo hiyo aliweza kuwashukuru wasanii mbalimbali aliyowashirikisha katika album hiyo akiwemo Mr Eazi, Yemi Alade, Sampa The Greatt, Burna Boy na vilevile amewashukuru Mashabiki wanaoendelea kumsupport.
Katika kipengele hicho alikuwa anachuana na
Best Global Music Album
- Voice Of Bunbon, Vol. 1 — Rocky Dawuni
- East West Players Presents: Daniel Ho & Friends Live In Concert — Daniel Ho & Friends
- Mother Nature — Angelique Kidjo
- Legacy + — Femi Kuti And Made Kuti
- Made In Lagos: Deluxe Edition — WizKid
Hii inakatisha tamaa kwa mashabiki wa Wizkid ambao kwa asilimia kubwa walikuwa wanaamini kwamba kipengele hiki kingechukuwa na mkali huyo kwani wengi tumeona mapokezi makubwa katika ile album yake iitwayo Made in Lagos.