Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa sababu za bei za mafuta kupanda ni pamoja na mgogoro wa kivita uliopo kati ya nchi ya Urusi na Ukraine na kupelekea kuwepo na uhaba wa upatikanaji wa mafuta duniani pia imepelekea gharama za mafuta na za usafirishaji mafuta kupanda.
Mkurugenzi wa Petroli wa Mamalaka hiyo Gerald Maganga amesema bei zilizotangazwa leo zitakazoanza kutumika kesho zimezingatia gharama zote halisi za mafuta ikiwa ni pamoja na ada ya mafuta ya shilingi 100 ambayo ilikuwa imesitishwa kuanzia mwezi December mpaka March.
Mafuta yanayopokelewa katika bandari ya Dar es Salaam kwa Petrol imepanda kutoka shilingi 2540 kwa lita kwa mwezi ulipita hadi shilingi 2861 kwa lita ikiwa ni ongezeko la shilingi 321. Kwa mafuta ya diesel yanayopita bandari ya Dar es Salaam yamepanda kutoka shilingi 2403 kwa lita mwezi uliopita hadi 2692 ikiwa ni ongezeko la shilingi 289.