Kutokana na taarifa ya kupanda kwa bei ya mafuta Nchini Waziri wa Nishati January Makamba anazungumza na Vyombo vya Habari jijini Dar es Salaam.
“mafuta yaliopo kwenye maghara na vituo Nchini na mafuta ambayo yanashushwa bandarini kwenye meli Nchini yanatosheleza kwa hakika kabisa mahitaji ya mafuta Nchini, hakuna uhaba wa mafuta Nchini na hakuna haja ya taharuki yoyote sababu tumeona jana baadhi ya watu wameanza kukimbia kwenye vituo nakujaza mafuta kwa wingi na kuleta taharuki”- Waziri Makamba
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Waziri Makamba anachozungumza muda huu kuhusu kupanda kwa bei Mafuta.