Mbunge wa Makete, Festo Sanga ametaka serikali kufanya mabadiliko ya sheria ya elimu ya mwaka 1978 ili kuondoa mwanya wa kila waziri anayeingia kwenye wizara hiyo kuamua anavyotaka.
Sanga ameyasema hayo leo Mei 10, 2022 akichangia bajeti ya Wizara yae elimu iliyowasilishwa na Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Adolf Mkenda.
Amesema “Hii sheria ya elimu ya mwaka 1978 ifanyiwe marekebisho, hii itaondoa mwanya wa Mawaziri wa nchi hii kuamua wanavyotaka kwenye elimu yetu.