Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amemvua mamlaka Makamu wake wa Rais, Saulos Chilima baada ya kutajwa katika kashfa ya ufisadi ya $ Milioni 150 (Tsh. Bilioni 349. 950) iliyohusisha kandarasi za Serikali.
Rais huyo amesema ripoti ya Taasisi ya Kupambana na Rushwa nchini humo (ACB) iliwataja Maafisa 53 wa sasa na wa zamani kuwa walipokea pesa kutoka kwa Mfanyabiashara kutoka Uingereza na Malawi Zuneth Sattar kati ya 2017 na 2021.
Hii ni kuhusiana na kandarasi 16 ambazo Huduma ya Polisi ya Malawi na Jeshi la Ulinzi la Malawi zilitoa kwa kampuni tano za Sattar, Maafisa waliotajwa kwenye ripoti hiyo ni pamoja na Makamu wa Rais na Mkuu wa Polisi ambaye amefutwa kazi.
Sheria ya Malawi hairuhusu Rais kumfukuza kazi au kumsimamisha kazi makamu wake kwakuwa Rais huyo ni Afisa aliyechaguliwa, Makamu wa Rais bado hajajibu tuhuma hizo.