Watumishi wanne wa serikali wakiwemo maafisa kilimo wawili kutoka wilaya Tandahimba Mkoani Mtwara wamesimashiwa kazi kwa tuhuma za kujaribu kuhujumu zoezi wa ugawaji wa pembejeo ambazo zinatolewa bure na serikali kama ruzuku kwa wakulima wa korosho nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigadia Jenerali Marco Gaguti amesema hayo wakati akishuhudia ushushwaji wa salpha ya unga tani 5632 kutoka kwenye meli bandarini Mtwara.
Gaguti amesema watuhumishi hao ni miongoni mwa watu 12 ambao wanashikiliwa na vyombo vya ulinzi kwa kosa la kujaribu kuchepushwa Lita 400 za salpha ambayo serikali ilitoa Kama ruzuku kwa wakulima wilayni humu.