Kiungo wa kimataifa wa Tanzania Novatus Dismas (19) amekamilisha usajili wake wa kujiunga na club ya SV Zulte Waregem ya Ligi Kuu Ubelgiji akitokea Maccabi Tel Aviv ya Israel akisaini mkataba wa miaka mitatu hadi 2025.
Novatus ni zao la Azam FC amelelewa na kukulia katika club hiyo na baadae akatolewa kwa mkopo kwenda Biashara United ya Mara kisha kuibuka mchezaji bora chipukizi 2019/2020 hapo Azam FC wakamrejesha na kuona anafaa kurudi kuwatumikia.
Mwaka huo 2020 akajiunga na Maccabi Tel Aviv akitokea Azam FC kwa mkataba ambao unawataka Maccabi kutoa asilimia 30 ya mauzo ya mchezaji huyo atakapouzwa lwenda club yoyote na sasa amejiunga na Zulte Waregen ya Ubelgiji kwa mkataba wa miaka mitatu.
Sasa inaripotiwa kuwa ameuzwa kwa euro 500,000 (Tsh Bilioni 1.2) kwenda Zulte Waregem kama kiasi hicho kimelipwa basi Azam FC wanavuta asilimia 30 yao ambayo itakuwa ni Euro 150,000 (Tsh milioni 367) kama sehemu ya mgao wao wa makubaliano ya kimkataba.