Waziri wa Nishati, January Makamba amefika kwenye Wilaya ya Makete Mkoa wa Njombe na kufika kwenye mradi wa kufua umeme kwa Njia ya Maji wa Rumakali (MW 222) wenye thamani ya Shilingi 1.4 Trilioni uliosanifiwa tangu mwaka 1998.
Mbele ya Waziri Makamba, Wananchi wamesema walishakata tamaa ya kuendelezwa mradi huo, Lakini kwa sasa matumaini hayo yamerudi na wanaamini utatekelezwa sababu Wananchi hao toka mwaka 1998 walikua tu wakisikia kwamba kuna mradi wa kufua Umeme lakini hakukua na mwendelezo au utekelezaji wowote kuhusu mradi huo.
Waziri Makamba amesema >>’Serikali imeamua kutekeleza mradi wa Umeme wa Maji ya Rumakali uliopo Wilayani Makete Mkoa wa Njombe ili kuwezesha nchi kuwa na Umeme wa kutosha kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya Nishati, kuanzia Agosti 1 2022 Wathamini wanakuja kuzungumza na nyinyi kuhusu maeneo tutakayoyachukua juu ya fidia zenu kwenye eneo hili la Kilometa za Mraba 13.2 zitakazochukuliwa na huo mradi’ – Waziri Makamba.