Serikali mkoani Manyara imesema itashirikiana na Wizara ya Maliasili na utalii kuhakikisha kunatolewa vitoweo vya wanyamapori kwa ajili ya kulipatia kabila la Wahadzabe ili wakubali kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na Makazi mwaka huu.
Hayo yamesemwa na mratibu wa sensa mkoa wa Manyara Gidion Mokiwa amesema katika zoezi la majaribio ya sensa serikali ilishatoa nyamapori kwa jamii hiyo ya Wahadzabe ili kutoa ushirikiano katika zoezi hilo.
Amesema kamati ya sensa kwa kushirikiana na ofisi ya mkoa wa Manyara tayari imeweka mchakato wa kuipatia jamii hiyo nyama pori ambapo kabla ya zoezi kuanza watawasiliana na viongozi wa mila za kabila hilo.
Aidha Mokiwa amesema Sensa ya kipindi kilichopita jamii hiyo iliomba kupatiwa nyama ya tembo hivyo mkoa kwa kushirikiana na maliasili waliweza kutekeleza hitaji lao ili kuweza kushiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi