Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dares Salaam limesema linatambua kuwa Jumamosi tarehe 13 Agosti 2022 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es salaam kutakuwa na mchezo wa soka wa Watani wa Jadi baina va Klabu ya Simba na Yanga zote za Dar es salaam utakaochezwa kuanzia saa 1:00 usiku.
•Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM Muliro Jumanne Muliro amesema “Katika kuelekea mchezo huo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dares salaam litachukua tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya mchezo, usalama utaimarishwa kwa kiwango cha juu”
“Ni marufuku kwa Mtu yeyote kwenda a silaha uwanjani isipokuwa vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo hilo, tunawatoa hofu Mashabiki watakaofika kushuhudia mchezo huo kuwa ulinzi ndani na nje ya uwanja utakuwa umeimarishwa kwa kiwango cha juu”