Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amebainisha Mikoa mitano Tanzania iliyopo katika hatari zaidi ya kupata Mlipuko wa Ebola.
“Tumebainisha Mikoa mitano ambayo ipo katika hatari zaidi ya kupata mlipuko wa Ebola mkoa wa kwanza ni Kagera, hii leo Katibu Mkuu wangu yupo Kagera kuangalia utayari wa Mkoa wa Kagera kukabiliana na mlipuko wa Ebola”
“Wengi tunafahamu mabasi yanatoka Mtukula Uganda yanaishia Mwanza kwa hiyo Mwanza inaingia namba mbili katika kuwa kwenye hatari zaidi lakini pia kuna Kigoma, Geita na Mara”
“Lakini tumebainisha zaidi kwamba Mikoa ya Dar es salaam, Arusha, Kilimanjaro, Songwe, Mbeya na Dodoma ipo katika hatari ya kati sababu ya uwepo wa Viwanja vya Ndege na vituo vikubwa vya mabasi kutoka nchi jirani”