Balozi wa zao la Pamba nchini Agrey Mwanri ambae awali aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora amesema vijana wengi hawajaona fursa zilizopo katika zao la Pamba huku wengi wakijikita kucheza Michezo ya bahati nasibu nakushindwa kuona fursa zilizopo.
Mwanri amesema hayo akiwa Mkoani Manyara wakati akizungumza na watendaji wa kata na Wakulima katika kampeni ya utekelezaji wa agizo la Rais Samia kufikia uvunaji wa tani Milioni moja hadi kufikia 2025 kupitia vipimo vyenye tija.