Azania Group ni moja ya chapa kubwa na maarufu ya bidhaa za chakula ambapo leo imezindua unga mpya wenye thamani na ubora wa hali ya juu na wenye ushawishi kwa watumiaji wake kutumia unga mweupe, laini na wenye kudumu kwa matumizi ya muda mrefu na kukidhi aina mbalimbali za mapishi ,Azania Group imezindua chapa yake mpya ya unga iliyopewa jina la AZANIA – PREMIUM HOME FOUR (PHF).
Akizungumza na Vyombo vya Habari Mkurugenzi wa Biashara wa Azania Group Bw Joel Laiser alisema….“Unga wetu mpya wa Azania PHF unakuja kama sehemu ya utafiti uliofanywa na kugundua uhitaji wake hivyo ili kuleta suluhu na kuleta utofauti kwenye soko na urahisi kwa watumiaji, Azania tumeendelea vyema kuja na bidhaa hii kwani mara nyingi watu wengi wanabanwa sana na muda na kushindwa kuzalisha bidhaa zenye ubora kama vile Maandazi, Chapati na vitafunio vingi zaidi na vya aina mbalimbali hivyo bidhaa yetu hii itatoa nafasi ya kuzalisha vitafunio vingi zaidi kuliko vile vilivyozoeleka. ”- Bw Joel Laiser
Uzinduzi huo ulipambwa na uwepo wa Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe.Jokate Mwegelo ambaye amepongeza juhudi za Azania Group katika soko la uzalishaji bidhaa za chakula.
“Nimefurahi kujumuika na Azania Group katika tukio hili adhimu na niwapongeze kwa kazi kubwa na mchango mkubwa wanaoutoa katika upatikanaji wa bidhaa za chakula na ,uthibitisho wake ni baada ya ujio wa bidhaa yao mpya ya Unga wa Ngano kwa ajili ya kupikia vitu mbalimbali kama vitafunwa na kurahisisha huduma na kazi za upishi kwa watumiaji mbalimbali hususani kwa mama zangu ambao ni Mama lishe lakini pia wanufaika(walaji) wengine na kipekee kabisa naomba niwashukuru kwa kuajiri idadi kubwa ya wafanyakazi kutoka katika wilaya yetu ya Temeke”- DC Jokate Mwegelo
Azania Group, imehitimisha kwa kusema “Unga wa Azania PHF utapatikana katika maduka yote Tanzania na yaliyopo mipakani, Sisi kama Azania group tutaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kutoa bidhaa bora, zenye suluhu za huduma kwa watumiaji wetu”
Uzinduzi huo umemalizika kwa wageni waalikwa wote kujivinjari kwa vitafunwa tofauti vilivyotengenezwa na Mama lishe kwa kutumia Unga mpya wa Azania PHF.