Mshambuliaji wa Galatasaray Didier Drogba amefanya kitendo ambacho kimezidi kumpa sifa kubwa linapokuja swala la kurudisha kwa jamii.
Drogba ambaye jana alitangaza rasmi kuondoka Galatasary baada ya mkataba wake wa miezi 18 kumalizika ametoa mchango wa zaidi ya billioni moja na nusu za kitanzania kwa familia za wahanga wa maafa yaliyotokea kwenye machimbo ya madini nchini Uturuki.
Drogba na wachezaji wenzake wa Galatasary walivaa ‘helmets’ kwenye mchezo wao wa mwisho wa ligi kuonyesha support juu ya tukio lilotokea machimboni ambapo raia huyu wa Ivory coast akachukua hatua nyingine ya ziada kuwasaidia wahanga wa maafa akiwa kama balozi wa Umoja wa Mataifa.
“Mimi ni balozi wa U.N na nitafanya kila kitu kusaidia watu waliopata maafa lakini sihitaji mtu yoyote atumie jina langu kujipatia umaarufu kupitia janga hili, mimi sio mtu wa kujipromoti kwenye vitu kama hivi.”
Tarehe 13 mwezi huu kwenye migodi ya makaa kulitokea mlipuko mkubwa uliosababisha vifo vya watu 301.
Kama unataka stori kama hizi zisikupite ungana na mimi kwenye twitter kwa kubonyeza HAPA, pia FACEBOOK & INSTA ili niwe nakutumia kila stori inayonifikia.