Shirika la APOPO kutokea nchini Ubelgiji ambalo limekuwa likitoa mafunzo mbalimbali kwa Panya katika nchini tofauti duniani ikiwemo Tanzania, limezindua mradi wa mafunzo maalum kwa Panya watakaosaidia zoezi la ukoaji pindi majanga ya asili yanapotokea kama vile kimbunga na tetemeko la ardhi.
Mradi huo umelenga kusaidia zoezi la ukoaji kwenye majanga ya asili baada ya manusura wengi kufariki kutokana na kushindwa kufikiwa na timu ya huduma ya ukoaji kwa kufunikwa na vifusi, hivyo mradi huo utahusisha teknolojia ya mafunzo maalum kwa Panya hao wataohusika kutafuta miili ya watu waliofunikwa na vifusi kisha kutoa taarifa kwa timu ya ukoaji.