Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Jumapili Novemba 6, 2022 amewasili Mkoani Kagera kushuhudia zoezi la uokoaji linaloendelea kufuatia Ndege ya Precision Air kupata ajali ilipokuwa ikikaribia kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba.

Aidha, Majaliwa amewajulia hali Wahanga wa ajali hiyo wanaopata matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera akiwemo Levina Theonest Lutinda na Mtoto wake Emmily Victor (pichani) ambao wote wameokolewa kutoka ndani ya ndege hiyo.
Akizungumza katika eneo hilo, Waziri Mkuu amesema Rais Samia Suluhu Hassan anatoa pole kwa wote walioguswa na ajali hilo na kwamba Serikali itaendelea kutoa huduma stahiki kwa majeruhi wote.
Tazama Ndege iliyoanguka Ziwa Victoria ilivyotolewa Ziwani, Majaliwa afika Hospitali