Meneja wa kiwanja cha ndege cha Arusha Mhandisi Elipid Tesha amesema kwa sasa ndege zinashindwa kutua usiku kutokana na kutokuwa na taa za kuongozea ndege kwa majira ya usiku lakini Serikali imetenga Tsh. Bilioni 2.2 kwa ajili ya jengo la kisasa “Kipindi cha high season ndege zinakuwa zaidi ya 145 lakini hivi sasa tunapata mapato ya Bilioni 1.3 kwa mwaka”
Akizungumza baada ya kukagua uwanja huo Naibu Waziri wa Uchukuzi amesema katika mwaka wa fedha ujao kiwanja hicho kitafungwa taa ili kuwezesha kiwanja hicho kufanya kazi usiku na mchana.