Rais wa Liberia George Weah pamoja na mkewe wamepata chakula cha jioni na mtoto wao Timothy Weah (22) kama sehemu ya kusherehekea goli la Timothy aliloifungia USA dakika ya 36 dhidi ya Wales katika mchezo wa sare ya 1-1 ya Kombe la Dunia nchini Qatar.
Timothy amechagua kuwa Raia wa Marekani kutokana na kuzaliwa New York 2000 ila mama yake ana asili ya Jamaica na Baba Liberia.
Baba yake ambaye kwa sasa ndio Rais wa Liberia toka 2018 George Weah ndio mchezaji wa pekee wa Afrika kuwahi kushinda tuzo ya Ballon d’Or 1995 (mchezaji bora dunia) lakini hajawahi kuipeleka Liberia kucheza Kombe la Dunia.