Tanzania ni Nchi pekee Afrika ambayo imetoa uraia kwa Wakimbizi 162,000 wa Burundi, 30,000 wa Rwanda na 10,000 wa Somali Bantus.
Mwakilishi wa Shirika la Wakimbizi Duniani upande wa Tanzania, Mahoua Parums ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa Ushirikiano kwenye masuala ya Wakimbizi katika kikao cha ndani alipokutana na Naibu Mwakilishi wa Kudumu Geneva Balozi Hoyce Temu @hoycetemu katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje.
•Ikumbukwe kuwa Ofisi za Uwakilishi wa Kudumu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Geneva inasimamia mashirika mengi ya Kimataifa ikiwemo UNHCR, Tanzania hadi leo hi inahifadhi Wakimbizi zaidi ya 260,000 mkoani Kigoma.