Kama gari halifiki basi tutakazia na boda, kama boda hazipenyi basi tutakazia na miguu…… ndivyo ilivyokuwa leo kwa Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Hamisi Taletale leo kuongozana na Waziri wa Maji Jumaa Aweso hadi saiti kunakojengwa mradi wa maji wa Morong’anya ambao utaleta sherehe kwa Wananchi zaidi ya elfu 52 kwenye Vijiji 19 utakapokamilika.
Pamoja na changamoto za barabara kuelekea eneo kilipo chanzo, Waziri Aweso na Mbunge wa Jimbo hilo Hamisi TaleTale na Viongozi wengine wa Chama walilazimika kutumia usafiri wa pikipiki kufika kwenye mradi huo unaojengwa kwa gharama ya Tsh. bilioni 23.1
Mbunge Taletale ambaye muda wote ameonekana kufurahishwa na mradi huu aliandika kwa hisia maneno ya shukrani kwa Rais Samia ———> “Sisi wana Morogoro Kusini Mashariki hatuna cha kumlipa Mheshimiwa Dr. Samia Suluhu Hassan zaidi ya kumpigania kwenye maombi na kulinda kura zake za mwaka 2025 kwa namna yoyote ili aweze kupata ushindi wa kishindo hapa Morogoro”