Mwenyekiti wa Jukwaaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile, amesema macho na masikio ya wadau wa habari nchini, yanaelekezwa jijini Dodoma kusubiri muswada wa Sheria ya Habari ukisomwa kwa mara ya kwanza Januari hii.
Balile amesema hayo leo tarehe 19 Januari 2023, katika ofisini za TEF, Kisutu jijini Dar es Salaam
“Mwezi huu tunatarajia kwamba wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari itawasilisha muswada wa huduma za Habari bungeni kama Waziri alivyoahidi mara kadhaa”
“Mungu akipenda mwezi Februari utakuwa umepitishwa na kuwa sheria basi tuanze huo utaratibu mwingine wa kuunda vyombo vinavyotakiwa ikiwemo baraza huru la habari, na utunzi wa kanuni zitakazokuwa zimetokana na mabadiliko mbalimbali”
Balile amesema kuwa ana imani kubwa na mchakato huo kwani maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan yanatekelezwa ipasavyo
“Tunaona maelekezo ya Rais Samia yanatekelezwa sasa na ni hamu yetu kuona kwamba muswada huo unaingia baada ya kushindikana bunge la Februari mwaka jana, ukashindikana mwezi wa tisa na mwezi wa 11”