Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo imetoa amri ya mwili wa Henry Massawe uzikwe katika eneo lake la makazi Kiaraka Magengeni, Bagamoyo mkoa Pwani.
Hukumu hiyo imetolewa January 24, 2023 na Hakimu Mkazi, Vedatus Mwalia ambaye alikubaliana na hoja za upande wa Ndugu wa marehemu waliotaka mwili wa Massawe uzikwe kwake.