Ikiwa hata bado hatujamalizana na mwezi Februari, na mwimbaji/mogul wa mitindo/kipenzi cha wengi ”RIRI”maarufu kama rihanna ambaye taarifa zake za hivi majuzi kuhusu ujauzito zilizo suprise wengi na kugonga vichwa vya habari zipo taarifa nyingine mpya kuwa sasa yeye na mpenzi wake Asap rocky wanajiandaa kufunga ndoa yao kwa siri huko barbados hivi karibuni.
Kama utakumbuka Rihanna alitumbuiza kwenye event ya Super Bowl,ndipo ndugu na mashabiki walishuhudia hali yake yakuwa ni mjamzito mtoto atakae kuwa wapili kwenye familia yao.
Kwa mujibu wa ripoti mpya kutoka kwa Radar Online, Rihanna na Rocky wanapanga kufunga ndoa siku za usoni na inaonekana wanandoa hao watabadilishana viapo katika nchi ya asili ya Barbados kwa siri.
“Kufanya harusi na kupata mtoto mwingine ndio jambo kuu la Rihanna kwa sasa,” chanzo hicho kilisema
Na ingawa anaweza kuwa anapanga albamu mpya au ziara ya tamasha, inaonekana kwamba mipango mingi ya siku zijazo ya RiRi inahusisha nyumba na familia.
“Amezungumza kuhusu kutaka watoto watatu au wanne kwa jumla,” mtu wa ndani anaongeza.
“Rihanna angependa kuwa na msichana baadaye – yeye na A$AP hata majina yamechaguliwa tayari.”