Shirika la afya duniani WHO limebaini kuwa idadi ya maambukizi iliripotiwa kupungua kwa asilimia 37 mwishoni mwa mwezi Februari lakini idadi ya vifo ikiwa haijapungua ambapo watu wasiopungua 81 wameripotiwa kufa kwa kipindupindu.
Mwezi uliopita, WHO ilionya kuwa Afrika inakumbwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa kipindupindu.
Nchi kadhaa za Afrika zinakabiliwa na milipuko ya kipindupindu, huku taifa la kusini mwa Afrika la Malawi likikumbwa na janga baya zaidi kuwahi kutokea.
WHO limesema jana kuwa idadi ya maambukizi ya kipindupindu imepungua kote barani Afrika.
Inakadiriwa kuwa kesi 26,000 na vifo 660 zimeripotiwa kufikia Januari 29, 2023 katika nchi 10 za Afrika zinazokabiliwa na milipuko tangu mwanzoni mwa mwaka, WHO ilisema.
Mnamo 2022, karibu kesi 80,000 na vifo 1,863 vilirekodiwa kutoka nchi 15 zilizoathiriwa.
Chanzo:UN.