Teknolojia inazidi kukua Duniani na Tanzania pia tunao Vijana wanaojimbizana nayo, @ayotv_ inakukutanisha na Mtanzania wa kwanza kuanzisha kituo cha kuzalisha vifaa vya kielektroniki (Smart Centre) Murtaza Ebrahim @thesalesimba ambapo safari amekuja na ubunifu wa teknolojia itakayouwezesha kufanya video conferencing na kupiga kura kidigitali kwa kuscan QR code huku matokeo yakionekana kwa uwazi kwenye Big Screen bila kuhitaji kutumia upigaji kua wa karatasi na masanduku.
Murtaza ambaye ni CEO wa Imperial Innovations @imperialinnovations ambayo inamiliki Smart Centre ya @morantanzania amesema mfumo huu unaweza kutumiwa kwenye shughuli mbalimbali za Kibunge, kwenye Mikutano mingine mikubwa, Vyuoni na maeneo mengine yanahohitaji kura ikiwemo kura za kuchagua Viongozi mbalimbali.
Mfumo huo uliopewa jina la Moran Experiential Hub unaweza kusaidia pia kufundishia Shuleni na Vyuoni, kufanyia mawasilisho mbalimbali (Presntention) na hata kufanyia uchambuzi wa Vipindi vya Michezo na Burudani kwenye Vyombo vya Habari.