Ingawa ilitoka taarifa ya Rais wa Malawi Bi.Joyce Banda kusitisha uchaguzi mpaka baada ya miezi 3,sasa kura za uchaguzi mkuu zinatarajwa kuhesabiwa upya hii leo katika maeneo ambapo imedhihirika kuwa idadi ya wapiga kura haiwiani na idadi ya wale waliojiandikisha kupiga kura.
Uchaguzi mkuu wa Malawi umezidi kuchukua sura mpya baada ya wanasiasa na wanasheria nchini humo kupeleka malalamiko yao mahakamani na kuzidi kuchelewesha matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika jumanne iliyopita.
Tume ya uchaguzi imekiri kuwa kuna maeneo kadhaa ambayo kuhesabu kwa kura kutarudiwa kwa sababu kura zilizopigwa zinazidi waliojisajili huku baadhi ya maeneo wamepiga kura mara 3 au mara 4 kama mji wa Mangochi waliosajiriwa ni watu 39,000 lakini kura zilizopatikana ni 180,000.