Katika mwendelezo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, leo Benki yetu ikiongozwa na Afisa Mkuu wa Uendeshaji, Bruce Mwile imefutirisha wateja na wadau wa benki wa visiwani Zanzibar, pamoja na vituo vya watoto yatima.
Hafla hiyo ya futari ilifanyika katika Hotel ya Verde na kuhudhuriwa na zaidi ya watu 400, ambapo mgeni wa heshima alikuwa Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga.
Tunaendelea kuwatakia waislamu wote nchini Ramadhani njema na kuwasisitiza kukithiri kufanya mema katika Mwezi huu Mtukufu na siku zote.