Baadhi ya wanadiplomasia na maofisa wa misaada nchini Afghanistan na duniani kote wameelezea wasiwasi wao kuwa huenda wafadhili nchini humo wakaondoa mpango wa misaada ya kibinadamu wa Afghanistan, ambao ni mkubwa zaidi duniani, kwani imeelezwa kuwa hadi sasa sababu kubwa ya kutekeleza mipango na kuwafikia wanawake katika nchi hiyo ya kihafidhina haingewezekana bila wafanyakazi wa kike huku Shirika la Umoja wa Mataifa la kutoa misaada ya kibinadamu likisema mpango mkubwa wa ufadhili kwa Afghanistan kwa mwaka 2023 unafadhiliwa chini ya 5%.
Utawala wa Taliban nchini Afghanistan umesema kuwakataza wanawake wa Afghanistan kufanya kazi katika Umoja wa Mataifa ni suala la ndani, baada ya shirika hilo la kimataifa kueleza kusikitishwa na uamuzi huo na kusema kuwa litapitia upya shughuli zake huko.
Katika tamko la kwanza la utawala wa Taliban kuhusu uamuzi huo tangu Umoja wa Mataifa ulipokubali kusikilizwa kwa vikwazo hivyo vipya wiki iliyopita, msemaji Zabihullah Mujahid alisema Jumatano sera hiyo inapaswa kuheshimiwa na pande zote.
Umoja wa Mataifa umesema hauwezi kukubali uamuzi huo kwani utakiuka katiba yake na imewataka wafanyakazi wake wote kutoingia katika afisi zake wakati ikifanya mashauriano na kukagua operesheni zake hadi Mei 5.
Siku ya Jumanne, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan ulisema utawala wa Taliban utawajibika kwa athari zozote mbaya za kibinadamu zinazotokana na marufuku hiyo.
“Ikiwa ufadhili hautapatikana kwa haraka, mamilioni ya Waafghanistan watakuwa wakitazama chini kwenye jaa la njaa, magonjwa na vifo,” .
Mamlaka ya Taliban mwezi Desemba ilisema wafanyakazi wengi wa kike wa NGO ya Afghanistan hawataruhusiwa kufanya kazi.