Tayari tumeona bondia Mayweather akitoa ushahidi wake kufuatia ugomvi mkubwa ulioibuka kati yake ya Rapa T.I juu ya usaliti na mke wake Tameka au Tiny na kusema Tiny ndie aliyesababisha kila kitu ambapo wapenzi hao hawakujibu chochote lakini sasa wameamua kuvunja ukimya kila mtu kwa wakati wake.
Kupitia Instagram, Tiny alianza kwa kuwashukuru mashabiki wake waliosimama pamoja nae na kuwaponda waliokuwa wakimsema lakini akafunguka kuwa mara nyingi mpenzi wake amekuwa akionekana na wasichana wengine lakini yeye alinyamaza tu hakusema chochote iweje watu wahoji baada ya yeye kuonekana na Mayweather?
Baada ya kukaa kimya kwa muda, Rapa T.I nae akaamua kujibu kupitia Instagram kuwa alijua ishu nzima baada ya kuambiwa kila kitu na kusema hajali tena lakini pia alionyesha kupitia video mkono wake akiashiria kwamba kweli aliingia katika ugomvi na mtu.