Jopo maalum la kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Nigeria litaanza kusikiliza kesi hiyo Jumatatu wiki ijayo.
Kesi hiyo iliwasilishwa kupinga ushindi wa rais mteule Bola Tinubu katika uchaguzi mkuu wa mwezi Februari.
Tinubu, kutoka chama tawala cha All Progressives Congress, aliwashinda wapinzani wake akiwemo Atiku Abubakar wa chama cha the People’s Democratic na Peter Obi wa chama cha Labour.
Walioshindwa wamedai kuwepo udanganyifu katika hesabu ya kura.
Hakuna kesi ya kupinga uchaguzi wa urais nchini Nigeria, imefanikiwa.
Majaji kutoka mahakama ya rufaa ndio watakaosikiliza kesi hiyo.