Baada ya mazungumzo ya muda mrefu na dili iliyosubiriwa kwa hamu, hatimaye kampuni ya kielektroniki ya Apple imethibitisha kuwa itanunua kampuni ya Beats Electronics watengenezaji wa headphones za Beats by Dre na bidhaa nyingine za muziki inayomilikiwa na mwanamuziki Dr. Dre.
Dili hiyo ambayo ina thamani ya jumla ya dola bilioni 3 inadaiwa kuwa ndio dili kubwa zaidi kubwa ya manunuzi kuwahi kufanywa na kampuni ya Apple.
Ikiwa ni sehemu ya manunuzi, wagunduzi wa kampuni hiyo Jimmy Iovine na Dr Dre wataungana na kampuni ya Teknolojia duniani Apple.
Bosi wa kampuni ya Apple Tim Cook amesema dili hiyo itaruhusu kampuni ya Apple kutengeneza bidhaa nzuri zaidi za muziki kupitia ugunduzi uliofanywa, teknolojia inayokuwa kwa kasi duniani.
Ungependa stori kama hizi zisikupite? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.